Saturday, January 24, 2009

NAMNA YA KUTUMIA BAMIA KAMA TIBA

Chimbuko la Bamia ni Abyssinia (Ethiopia) Kisha ikaenea Duniani kote.

1. Michirizi na utonvu unaopatikana katika Bamia, husaidia kusawazisha Kisukari kwa kuzuia kiwango cha Sukari inayotumika katika mwili kutoka kwenye utumbo mkubwa.

2. Utelezi wa bamia huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali (cholesterol) na asidi ya Nyongo unaoingia kutoka kwenye Ini ambao usipo dhibitiwa huenda ikasababisha matatizo ya ki-afya.

3. Bamia husaidia kulainisha Utumbo mkubwa (large intestines) kutokana na kazi yake ya kulainisha choo.

4. Bamia hutumika kwa kutibu vidonda vya Tumbo inasaidia kusawazisha Asidi.
Magonjwa Maalum

Asidi ya Kujirudia rudia na Kufunga Choo

Tafuna vipande sita vya Bamia bila kutumia dawa nyigine kilasiku na Asidi ya Kujirudia rudia na kufunga choo kutakwisha, inashusha Sukari kutoka 135 hadi 98

Pumu
Bamia ina Vitamin C ambayo inawafana watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe ya Bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya vitamin C.

Kidonda Ndugu (Cancer)
Bamia husaidia kuweka Utumbo kuwa na hali nzuri hivyo kupunguza uwezakano wakuugua ugonjwa huu wa Kansa hasa kwenye utumbo mkubwa.

Mishipa midogo ya Damu Kula Bamia kwa wingi kunasaidia kuimarisha Mishipa midogo ya Damu.

Cataracts
Nusu kikombe cha Bamia iliyopikwa inakua na kiwango cha 460 IU ya vitamin A.ambayo inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataracts).
Usongo (Depression) na Kukosa Nguvu. Bamia ni mboga bora zaidi kwa wale wanaojisikia dhaifu, Kuchoka na wanao athirika na Usongo (depression).

Usalama:
Hakuna hali yoyote ya tahadhari inyojulikana kwa kutumia mboga hii.

3 comments:

  1. Asante kwa maelezo mazuri kuanzia sasa nitakula bamia mpaka basi!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Asante kwa maelekezo yk tutayafanyia kazi

    ReplyDelete