Saturday, January 24, 2009

FUNGA NDOA KIURAHISI KUPITIA NYOTA

NYOTA YA PUNDA NA MIZANI

Mpate mpenzi siku ya Ijumaa kwenye sherehe za ngoma saa 3 au saa 9, vaa nguo rangi mbili juu nyekundu chini njano. Mshike mkono mara kwa mara, hakikisha mnakula kabla ya mazungumzo


NYOTA YA NGOMBE NA NGE

Ng’ombe: kutana nae saa nane na uwe peke yako, Vaa nguo ya rangi ya kijani iwe siku ya Jumanne saa 2 au saa 8. Mpe chakula cha mafuta mafuta na rojo rojo. Mkutanishe na jamaa zako wa nyumbani usimtazame usoni, mguse guse shingo na mapaja. Penda kuimba imba au vaa Walkman. Tendo la ndoa liwe refu na la kurudia rudia.

NYOTA YA MAPACHA NA MSHALE

Penda sana kuzungumza kiingereza au kusoma soma na kushika gazeti unapotembea mbele yake. Kutana nae siku ya Jumatano saa 9 na mpende ndugu yake wa pili. Penda kutafuna tafuna Big G na zungumza utani kwa wingi huku ukizungumza upesi upesi. Vaa nguo za kitoto fupi na usikose mkanda.

NYOTA YA KAA NA MBUZI

Penda sana kununa, usicheke hovyo, mpe vitu baridi kama peremende, ice cream, na vitu vya kunyonya. Mvamie na umshike shike kitovu pia mfinye finye vidole. Tembea nae taratibu na uzungumze nae pole pole, penda sana mambo yake. Vaa nguo ya rangi ya bluu isiyoiva. Lazima muishi sehemu za bondeni na nyumba yenu iwe na choo cha ndani na sehemu ya kulia chakula. Kutana nae Jumamosi au Jumapili saa 4 au saa 10. Zungumza nae kwa kigugumizi.

NYOTA YA SIMBA NA NDOO

Mpenzi apende kukandwa na kutolewa ukali na mtembee kwa haraka, saa za mapumziko ziwe saa 1 na saa 5. Awe muhongaji na mkae karibu na nyumba ya kona. Mwanamke avae Kofia au Ushungi na kiuno akibane kwa Mshipi au kanga. Tendo la ndoa liwe fupi na la kurudia lakini pendelea kukandana. Kutana nae siku ya Jumapili ambayo ndio siku ya Mapenzi.

NYOTA YA MASHUKE NA SAMAKI

Chagua mpenzi asiesoma zaidi kuliko aliyesoma, utampata mpenzi wa ndoa tarehe 30 na huenda mkakutan hospitali au hotelini au baada ya ajali. Kuwa maridadi, viatu virefu vya kisigino na mlio. Usikose senti ndogo na uoneshe kulia au kukata tamaa na kumuhudumia katika ugonjwa wake au jamaa wake wa kike. Kutaneni siku ya Alhamisi.

No comments:

Post a Comment