Saturday, January 24, 2009

JUA MAANA YA NAMBA YAKO YA SIMU

Unapotaka kutafsiri namba yako ya simu tumia tarakimu nne za mwisho kwani hizi ndizo namba pekee ambazo ni tafauti na za watu wengine katika mtandao mmoja.
Jumlisha tarakimu hizo nne hadi ufikie jumla ya tarakimu moja (single digit) yaani jumla iwe kati ya 1 na 9.

JUMLA IKIWA 1
Hii ni namba yenye nguvu sana na ni namba ya kiume, ambayo inakuza nguvu zako binafsi ambayo inakuwezesha pia kuwashawshi watu wengine. Tahadhari usiwe mbabe kwa watu. Hii pia ni namba nzuri sana kwa biashara na kazi lakini sio namba nzuri ya aliye mpweke kumtafuta mpenzi.

JUMLA IKIWA 2.
Hii ni namba ya mapenzi, ni namba nzuri kwa walio wapweke kutafuta wapenzi. Namba hii inaashiria hisia, mawasiliano ya kibusara na ushirikiano, pia ni namba nzuri ya biashara ya huduma na sio nzuri kwa madalali na watu wabishi.

JUMLA IKIWA 3
Namba hii inaashiria ubunifu, ucheshi, hii ni namba nzuri kwa wasanii, wanamziki na vijana. Namba hii haina muelekeo lakini ina mvuto na ni asilia. Ni namba nzuri sana kwa waandishi na watunzi wa nyimbo sio namba nzuri sana kwa watu wanaojituma sana na wenye malengo makubwa.

JUMLA IKIWA 4
Hii ni namba thabiti, iliyostawi, yenye kutegemewa na kuaminika, namba hii ni nzuri sana hasa kwa ma Benki, makampuni ya Uhasibu, Sheria na makampuni au masharika mengine kama hayo ambayo yanahitajika kua waaminifu na sifa za kuaminika. Pia ni namba nzuri kwa familia kubwa na wala sio nzuri kwa watu walio wapweke (Singles) vinginevyo wawe ni wanasharia au wahasibu au Wafanya kazi za kibenki.

JUMLA IKIWA 5
Namba hii inaashiria matukio na mabadiliko ni namba liyo tulia. Tegemea usioyatarajia ni namba nzuri ya kufanya mauzo pia ni namba nzuri kwa wasafiri wanaopenda uhuru wao. Sio namba nzuri kwa familia kwani inakosa hadhi ya heshima na kuwajibika na vile vile sio namba nzuri kwa wanaopenda kula hovyo au wategemezi wa aina yoyote.

JUMLA IKIWA 6
Hii ni namba nzuri sana kwa familia kwani ni namba inayoashiria kujali, ulinzi na inaunganisha familia na kudumisha uhusiano wa kirafiki na kifamilia. Sio namba nzuri walio wa pweke.

JUMLA IKIWA 7
Strong and spiritual, this number is ideal for scholars and free thinkers. Also improves mental health and stability. Not a good number for business.

JUMLA IKIWA 8
Hii ni namba nzuri sana kwa biashara yoyote. Namba hii huvuta pesa na utiifu. Pia n namba nzuri sana kwa wanaojituma sana katika kazi huboresha wadhifa wako na kipato chako katika.

JUMLA IKIWA 9
Hii ni namba nzuri sana katika kazi au huduma za kiafya au taasisi zisizo za kibiashara. Hii ni namba yeye bahati kuliko namba zote kwani wakati mwingine huweza kukuletea kipato cha juu usichokitegemea sio namba namba nzuri kwa wale wenye matatizo ya kiafya.

2 comments:

  1. Replies
    1. Chukua namba au tarakimu 4 za mwisho wa namba yako ya simu kisha jumlisha hizo namba mpka upate tarakimu moja. Yan kw mf 4+1+7+1=13; tna chukua 1+3=4. Then angalia maana

      Delete